COMMIPHORA; DAWA INAYOFANYIWA UTAFITI SUA NA INAYOLETA MATUMAINI DHIDI YA VIDONDA SUGU

Commi cream

Wataalamu wa afya katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo wanafanya utafiti wa dawa ya asili inayotokana na mti wa Commiphora (Commiphora swynnertonii)

Utafiti huo ambao unaongozwa na Dr Gaymary Bakari (PhD) na Dr Shaban Mshamu umekuwa ukitoa matokeo yanayoleta matumaini juu ya ubora wa dawa hiyo dhidi ya vidonda sugu na matatizo mengine ya ngozi.

Commi cream

 

Mti wa Commiphora umekuwa ukitumika kama chanzo cha dawa kwa matatizo mbalimbali ya binadamu na wanyama na jamii tofauti nchini hasa wamasai.

Kufanyika utafiti katika maabara za kisasa za idara (Department of Physiology, Biochemistry and Pharmacology), kunafungua ukurasa mpya na muhimu unaoleta matumaini makubwa kwa wagonjwa na wataalamu wa afya nchini

 Commi spray

Kwa sasa utafiti wa dawa hii upo katika hatua mbalimbali za majaribio na bidhaa tofauti zimeandaliwa zikiwa na kiambata cha Commiphora na zinazotumika kama dawa. Baadhi ya bidhaa zipo katika mfumo wa lotion, sprays, cream, sabuni na kadhalika.

Matumizi ya mti wa commiphora ambao huitwa majina tofauti na jamii tofauti nchini na nje ya nchi ni ya muda mrefu. Ni mojawapo ya miti inayoaminika kuwa na aina tofauti za viambata zinazoweza kutibu magonjwa mbalimbali kwa binadamu na mifugo

Ni matumaini ya idara na chuo kwa ujumla kwamba matokeo ya utafiti huu yatainufaisha jamii katika kupambana na magonjwa, hasa katika kipindi hiki baada ya kuongezeka kwa usugu wa vimelea dhidi ya dawa nyingi za viwandani.

 Rotavapour

Mojawapo ya mashine ya kisasa inayotumika katika utafiti huo, kwenye maabara ya idara

Related Posts