IDARA YAFAIDIKA NA UFADHILI WA POLISH AID

Mradi wa ukarabati wa maabara katika Ndaki ya Tiba ya Mifugo na Sayansi za Afya unaotekelezwa na shirika la Foundation Science for Development umegusa idara ya Fiziologia, Biochemia na Famakolojia. Katika ukarabati huo, maabara ya kufundishia kwa vitendo (MLB 8) inayosimamiwa na idara imefanyiwa maboresho makubwa na muhimu.

MLB 8 renovation 1 condensed

 

MLB 8 renovation 2 condensed

Miongoni mwa maboresho yaliyofanyika ni kuwekwa kwa sakafu na meza za marumaru, madirisha ya kisasa na kuwekwa mfumo wa kupoza (kiyoyozi). Aidha maabara hiyo imewekwa ubao wa kisasa na vifaa vya kufanyia projection.

Launching group at MLB 8 condensed

Mkuu wa Idara ya Fiziolojia, Biokemia na Famakolojia, Dr Gaymary Bakari amewaongoza wafanyakazi wa idara kushiriki katika hafla ya kuzinduliwa maabara hizo iliyofanyika tarehe 26/11/2020.

SHARE THIS INFORMATION WITH YOUR FRIEND