BODI MPYA YATEMBELEA NA KUJIONEA MAENDELEO YA UKARABATI MKUBWA UNAONDELEA WA MAJENGO NA MIUNDOMBINU MBALIMBALI ILIYOPO NDAKI YA TIBA ZA WANYAMA NA SAYANSI ZA TIBA

Bodi mpya ya Ndaki ya Tiba za Wanyama na Sayansi za Tiba, iliyoanza majukumu yake kuanzia mwezi Juni mwaka huu;  leo tarehe 29 mwezi Septemba kabla ya kuketi kikao chake cha kawaida cha 16, imetembelea na kujionea ukarabati mkubwa wa majengo na miundombinu mbalimbali unaondelea ndani ya Ndaki ya Tiba za Wanyama na Sayansi za Tiba. Ziara hiyo ilijumuisha Mwenyekiti wa Bodi Dr. Henry Mbwille ambaye aliongoza wajumbe wengine wa Bodi hiyo akiambatana na Rasi wa Ndaki Professa Elliot Phiri pamoja na watendaji waandamizi wa Ndaki.

Katika ziara hiyo Bodi ilipongeza na kuishukuru Serikali kwa kugharamia ukarabati huo na pia kuwapongeza watendaji wa Ndaki kwa kuendelea kuchapa kazi kwa ufanisi licha ya changamoto za muda mfupi zilizopo zinazotokana na wao kuondoka katika ofisi zao kupisha ukarabati.

Katika kikao chake cha 16 cha kiutendaji, Bodi ilipokea na kujadili ripoti mbalimbali za maendeleo ya Ndaki ikiwemo maboresho mbalimbali ya maabara za kfundishia uliokwisha kufanyika na unaondelea kufanyika hivi sasa.

“Ukarabati huu utaboresha mazingira ya kusomea kwa wanafunzi pamoja na kuweka mazingira bora ya kufanyia kazi kwa wanataaluma pamoja na wafanyakazi wengine wote”

Sambamba na hilo Bodi ilipongeza juhudi za Chuo na Serikali kutoa fursa zaidi za masomo kwa wahitimu wa Sekondari na vyuo vya kati kupitia kuongeza udahili na pia kwa kuendelea kutoa wahitimu bora.

Bodi iliahidi katika kipindi chake cha miaka mitatu ijayo ya utendaji wake itaendelea kusimamia na kushirikiana kwa karibu na Menejiment ya Ndaki na SUA kwa ujumla ili kutatua changamoto zilizobakia ili Ndaki iendelee kuwa bora na mfano kwa vyuo vingine.

Mabli na Dr. Henry Mbwille ambaye ni Mwenyekiti na ambaye atashika wadhifa huo hadi Desemba 2022, wajumbe wengine wa Bodi hiyo ni wafuatao:

 

WAJUMBE WALIOTEULIWA TOKA TAASISI ZA UMMA

1. Professa Mohamedi Janabi ambaye ni Mkurugenzi wa taasisi ya moyo ya Mh. Jakaya Kikwete (Director, Jakaya Kikwete Cardiac Institute) (ameteuliwa kwa kipindi cha pili)

2. Dr. Bedan Masuruli ambaye ni Msajili wa Baraza la Madaktari wa Wanyama Tanzania (Registrar, Veterinary Council of Tanzania) (ameteuliwa kwa kipindi cha pili)

 

WAJUMBE WALIOTEULIWA TOKA SEKTA BINAFSI

1. Dr. Emmanuel M. Swai

2. Dr. Jerome B. Bahemu

 

WAJUMBE WA NDANI YA NDAKI WANAOWAKILISHA MAKUNDI MBALIMBALI

1. Dr. Claudius Luziga ambaye anawakilisha wanataaluma (amechaguliwa na wanataaluma kwa kipindi cha pili)

2. Ndugu Alfred G. Mwanyika ambaye anawakilisha wafanyakazi wasaidizi wa wanataaluma)

3. Mrs. Enesa Mlay ambaye anawakilisha wafanyakazi waendeshaji (amechaguliwa kwa kipindi cha pili)

4. Ms Nonyane P. Uvanna ambaye anawakilisha wanafunzi wa ndani ya Ndaki

 

Pia wapo wajumbe waalikwa ambao ni wakuu wa idara pamoja na wenyeviti wa kamati mbalimbali za utendaji ndani ya Ndaki

Related Posts