HOSPITALI YA RUFAA YA WANYAMA SUA YAFANYIWA UBORESHAJI KUIMARISHA HUDUMA

front view

front view

Jengo la hospitali ya rufaa ya wanyama SUA

Hospitali ya rufaa ya wanyama SUA ndiyo hospitali pekee ya hadhi ya rufaa kwa wanyawa nchini Tanzania. Hospitali hii ambayo ipo chini ya College ya Tiba za Wanyama na Sayanzi za Afya katikaChuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo imekuwa msaada mkubwa kwa wafugaji nchini katika kutatua shida mbalimbali za afya ya wanyama.

 Kibao 2

Muda wa kazi katika hospitali ya rufaa ya wanyama ya SUA

Hivi karibuni hopitali hii imeingia katika programu ya ubioreshaji ikihusisha upanuzi wa jengo na uboreshaji wa vifaa-tiba. Dr Isack Kashoma ambaye ni mratibu msimamizi wa hospitali hii amebainisha kwamba uboreshaji uliofanyika na unaoendelea kufanyika ni hatua muhimu katika kuhakikisha huduma kwenye hospitali hiyo zitakuwa za kiwango cha juu zaidi. Uboreshaji wa hospitali hii umewezeshwa na fedha za serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na msaada wa shirika la “Foundation Science for Development” kwa ufadhii wa serikali ya Poland.

renovation 2Kashoma 2

Dr Isack Kashoma akitoa maelezo kuhusu shughuli za hospitali

 

Hospitali ya rufaa ya wanyama SUA hutumika pia kama hospitali ya kufundishia kwa wanafunzi wanaosoma masomo ya tiba za wanyama chuoni SUA. Dr Kashoma amesema kuwa uboreshaji wa hospitali utasaidia kuboresha huduma za kufundisha wanafunzi kwani utasaidia uwepo wa eneo kubwa zaidi la kufundishia na vifaa bora na vya kisasa zaidi.

Haematological analyser

 Mashine maalumu ya kuchukua vipimo vya damu (Haematological analyzer) kwa ajili ya kupima afya ya wanyama

Hospitali ya rufaa ya wanyama SUA inajikita katika huduma mbali mbali ikiwemo matibabu ya kawaida ya wanyama, upasuaji, chanjo na ushauri kwa wafugaji. Hospitali hii ina wodi maalumu kwa ajili ya kulaza wagonjwa (wanyama) wanaohitaji uangalizi wa karibu.

urine analyzer 2

Mashine maalumu ya kuchukua vipimo vya mkojo (urine analyzer) kwa ajili ya kupima afya ya mnyama

Related Posts