Matukio Mbalimbali yaliyojiri wakati wa Kongamano la kwanza nchini Tanzania kuhusu Afya Moja (One Health) likihusisha wadau toka sekta mbalimbali hususan mifugo, afya, kilimo na mazingira

Dr Faustine Ndungulile

Dr Faustine Ndungulile

Naibu Waziri wa Afya Dr. Faustine Engelbert Ndugulile akizungumza na wadau wa afya moja katika hafla ya ufunguzi wa kongamano la kwanza la wadau wa afya moja lililoandaliwa kwa pamoja kati ya chama cha madaktari wa wanyama Tanzania (TVA) na Ofisi ya Waziri Mkuu. Waliokaa upande wa kushoto wa Muheshimiwa Naibu Waziri ni Msajili wa Baraza la Wataalam wa Afya ya Wanyama (VCT) na mwakilishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dr. Bedan Masuruli, akifuatiwa na Makamu Mkuu wa Chuo cha Kilimo cha Sokoine Professa Raphael Chibunda na Mwenyekitii wa chama cha Madaktari wa wanyama Professa Dominic Kambarage

 

Kanali Jimmy Matamwe

Kulia Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Shughuli za Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu kanali Jimmy Matamwe akitia neno la ubani wakati wa hafla ya ufunguzi wa kongamano la kwanza la wadau wa afya moja. Waliokaa kutoka kulia ni Msajili wa Baraza la Wataalam wa Afya ya Wanyama (VCT) na mwakilishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dr. Bedan Masuruli, akifuatiwa na Makamu Mkuu wa Chuo cha Kilimo cha Sokoine Professa Raphael Chibunda na Mwenyekitii wa chama cha Madaktari wa wanyama Professa Dominic Kambarage na upande wa kushoto ni Naibu Waziri wa Afya Dr. Faustine Engelbert Ndugulile

4

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Professa Raphael Chibunda akisisitiza jambo wakati wa hafla ya ufunguzi wa kongamano la kwanza la Afya Moja lililofanyika Nomba 27 hadi 29 mwaka 2019 katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Arusha (AICC)

Professor Dominic Kambarage

Mwenyekitii wa chama cha Madaktari wa wanyama Professa Dominic Kambarage akiongea na kusisitiza jambo muda mfupi kabla ya kuanza kwa kongamano la kwanza la afya moja lililofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Arusha (AICC). Pembeni yake kushoto ni Msajili wa Baraza la Wataalam wa Afya ya Wanyama (VCT) na mwakilishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dr. Bedan Masuruli, akifuatiwa na Makamu Mkuu wa Chuo cha Kilimo cha Sokoine Professa Raphael Chibunda na Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Shughuli za Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu kanali Jimmy Matamwe

5

Mdau na mtafiti mwandamizi toka ndaki ya Tiba ya Wanyama, SUA Professor Robinson Mdegela (aliyesimama) akiwasilisha mada kuhusu dhana ya Afya Moja.

IMG E5271

Mtafiti toka SACIDS Dr Leonard Mboera (aliyesimama) akifafanua jambo kuhusu mchango wa wadau mbalimbali ikiwamo SACIDS katika kuimarisha ushirikiano wa kisekta na dhana nzima ya afya moja

IMG E5205

Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Shughuli za Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu kanali Jimmy Matamwe (kulia), Mkurugenzi wa Taasisis ya utafiti wa magonjwa ya binadam Professor Yunus Mgaya (katikati) na aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha madaktari wa Wanyama Tanzania ambaye ni mtafiti mwandamizi na mdau wa afya moja toka chuo kikuu cha kilimo cha Sokoine Professa Rudovick Kazwala (kushoto) wakifuatilia kwa makini mijadala inayoendelea wakati wa kongamano la kwanza la Afya Moja lililofanyika Nomba 27 hadi 29 mwaka 2019 katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Arusha (AICC)

Wajumbe wa Afya Moja 3

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya kongamano la kwanza la Afya Moja lililofanyika Nomba 27 hadi 29 mwaka 2019 katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Arusha (AICC). Kutoka kushoto ni muhadhiri kutoka ndaki ya Tiba za Wanyama, SUA, mwenyekiti wa kamati ya Kisayansi ya TVA na Muhariri mkuu wa Jarida la Kisayansi la Vetenari Tanzania (Tanzania Veterinary Journal), Dr. Augustine Matondo (PhD). Katikati ni Dr. Zachariah Makondo (PhD) ambaye ni makamu mwenyekiti wa kamati ya Kisayansi ya TVA na Muhariri mshiriki wa Jarida la Kisayansi la Vetenari Tanzania (Tanzania Veterinary Journal). Kulia ni Katibu Mkuu wa chama cha Madaktari wa wanyama (TVA) na  Dr. Henry Magwisha (PhD) (anayeandika) na upande wa nyuma ni wajumbe mbalimbali toka sekta binafsi na taasisi za umma wakiongozwa na Professa Robert Maselle toka ndaki ya Tiba za wanyama SUA

IMG 5618 1

Wajumbe wakifuatilia kwa makini mijadala wakati wa kongamano la kwanza la Afya Moja lililofanyika Nomba 27 hadi 29 mwaka 2019 katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Arusha (AICC)

IMG 5622

Wajumbe wakifuatilia kwa makini mijadala wakati wa kongamano la kwanza la Afya Moja lililofanyika Nomba 27 hadi 29 mwaka 2019 katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Arusha (AICC). Wa kwanza mstari wa nyuma kutoka kushoto ni muhadhini wa TVA Dr Caroline Uronu

IMG 5623

Wajumbe wakifuatilia kwa makini mijadala wakati wa kongamano la kwanza la Afya Moja lililofanyika Nomba 27 hadi 29 mwaka 2019 katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Arusha (AICC).

IMG E5267

Wajumbe wakiwa ukumbini mda mfupi kabla ya kuanza kongamano la kwanza la Afya Moja lililofanyika Nomba 27 hadi 29 mwaka 2019 katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Arusha (AICC).

Wajumbe wa Afya Moja

Wajumbe wakiwa ukumbini mda mfupi kabla ya kuanza kongamano la kwanza la Afya Moja lililofanyika Nomba 27 hadi 29 mwaka 2019 katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Arusha (AICC).

 

Related Posts