Serikali ya Tanzania imekipongeza chama cha madaktari wa mifugo Tanzania TVA

Professor Hezron E.Nonga

Serikali ya Tanzania imekipongeza chama cha madaktari wa mifugo Tanzania TVA na wanachama wake kwa jitihada mbalimbali inazozifanya katika kusaidia kuhakikisha sekta ya mifugo inatoa mchango unaostahili kwa jamii na katika pato la Taifa.

Professor Hezron E.Nonga

Mkurugenzi wa huduma za Mifugo Tanzania kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Hezron Nonga (Katikati) Akizuzungumza wakati wa kufunga Mkutano wa kwanza wa wadau wa afya moja (afya shirikishi), Kushoto ni Prof. Dominic Kambarage Mwenyekiti wa TVA na Kulia ni Betha Dugange Afisa Mifugo Mkuu,Idara ya ya Uratibu wa Sekta TAMISEMI aliyemuwakilishi wa Mkurugenzi TAMISEMI

Pongezi hizo zimetolewa na Mkurugenzi wa huduma za mifugo Tanzania kutoka wizara ya Mifugo na uvuvi Prof. Hezron Nonga wakati akifunga mkutano wa mwaka wa TVA na kongamano la kisayansi uliozungumzia dhana ya fya moja ambayo pia hujulikana kama afya shirikishi, kongamano ambalo limewakutanisha wadau wa mifugo,Kilimo,Mazingira,TAMISEMI,na Wizara ya afya lililofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa jijini Arusha IACC .

Prof. Nonga amesema tafiti mbalimbali za kisayansi zilizowasilishwa kwenye mkutano huo zimesaidia sana kujengeana uwezo miongoni mwao lakini pia kwa wadau wengine ambao sio wataalamu wa mifugo lakini ni wadau wa dhana ya afya moja katika kujua namna magonjwa hayo ya kuambukiza kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu yanavyotokea na namna ya kuyadhibiti kwa pmoja wa ushirikiano.

” Tunasema mfano mchango wa sekta ya mifugo upo chini  ya asilimi 7.4 ya GDP  bado hakuna tafiti zilizofanywa kuonyesha mazao ya mifugo kama vile nyama,maziwa,mayai na samaki vinachangia Protini Kiasi gani katika lishe ya binadamu hivyo ni muhimu tafiti za aina hii pia zifanyike ili tujiridhishe kuhusu mchango mdogo wa sekta kama inavyosemwa” Alisema Mkurugenzi huyo wa huduma za mifugo Tanzania Prof. Nonga

Prof. Nonga amesema Mkutano huo wa kwanza wa dhana ya afya moja umesaidia kuwajengea uwezo wadau wa sekta mbalimbali wanaunda dhana hiyo kupata uelewa wa pamoja na kuona umuhimu wa ushirikiano huo katika kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali ambazo zinahitaji ushirikiano wa sekta zaidia ya moja na hivyo kuisaidia serikali katika kupanga mipango yake ya maendeleo na pia katika kutimiza agenda hiyo ya dunia.

Ameongeza kuwa sekta ya mifugo inakabiliwa na changamoto nyingi ambazo wadau hao kupitia kongamano hilo lililoandaliwa kwa ushirikiano kati ya TVA na ofisi ya Waziri Mkuu wameweza kuzizungumzia kwa pamoja kama wataalamu wa Mifugo na kuweka mikakati ya namna ya kuzitatua hali ambayo inasaidia utekelezaji wa majukumu ya wizara ya mifugo baada ya kupata ushauri wa wataalamu hao waliobobea kwenye sekta hiyo.

” Nawapongeza sana kwa majadiliano mazuri mfano kwenye upande wa utoaji wa chanjo za mifugo, tunampango wa kuzalisha chanjo nyingi sawa lakini bila kujua mbinu bora za utoaji na usambazaji wa chanjo hizo tutajikuta tunakwama kama ambavyo tulikwama kwenye utoaji wa chanjo ya homa ya mapafu ya ng’ombe lakini nyinyi mmetushauri vyema kabisa kwenye mkuatano huu ushauri ambao serikali tunakwenda kuufanyia kazi ili kuleta tija” Alisema Prof. Nonga.

Amesema kuwa Wizara kupitia  kurugenzi yake itahakikisha inasaidia mifugo ya nchi hii inakuwa salama na kustawi inavyotakiwa na kutokuwa chanzo ya magonjwa yanayotoka kwa mifugo kwenda kwa binadamu na hivyo kuwezesha nyama ya Tanzania kwenda nje ya nchi kitu ambacho hakifanyiki kwa sasa kutokana na magonjwa mifugo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mdaktari wa Mifugo Tanzania TVA  Prof. Dominic Kambarage ameshukuru muitikio mzuri wa wadau wa afya moja kwenye mkutano huo muhimu na wa kwanza nchini na kutumia fursa hiyo kuomba ushirikiano zaidi katika utekelezaji wa dhana hiyo ya afya moja kwa sekta zote.

Prof. Kambarage ameomba viongozi wa Wizara ya Mifugo na uvuvi,TAMISEMI,Utumishi kusikiliza changamoto za wataalamu hao ambazo zinakwamisha utendaji wao ili waweze kufanya kazi kwa moyo na hivyo kulisaidia taifa kupitia taaluma zao badala ya kufanya kazi wakiwa na malalamiko mbalimbali yanayopunguza ari yao ya kazi.

Mwenyekiti huyo wa TVA amesema mada mbalimbali za kisayansi zimewasilishwa kutoka kwa watafiti katika sekta mbalimbali ikiwemo Kilimo, Afya,Tasisi za elimu ya juu na taasisi za utafiti ambazo zimesaidia kujenga uelewa wa pamoja juu ya changamoto zinazoikabili sekta ya mifugoafya na mazingira na hivyo kuweka maazimio ya namna ya kuzitatua kwa maslahi mapana ya wananchi na taifa.

Mwenyekiti huyo wa TVA pia alitoa shukrani zake za dhati kwa wadau mbalimbali toka sekta binafsi na za umma ambao wamewezesha kongamano hilo la kwanza na la kihistoria kufanyika hapa Tanzania na kuvutia washiriki mbalimbali toka hapa nchini ina duniani kote

Related Posts