WAHADHIRI VET WAPONGEZWA KWA KAZI KUBWA WANAYOFANYA

Dr Mbwile 1

Dr Mbwile 1

Dr Henry Mbwile, Mwenyekiti wa Bodi ya Ndaki ya Tiba ya Wanyama na Sayansi za Afya

Mwenyekiti wa Bodi ya Ndaki (College board) ya Tiba ya wanyama na Sayansi za Afya, Dr Henry Mbwile amewapongeza wahadhiri na wafanyakazi wote katika ndaki hiyo kwa kazi kubwa wanayofanya kuhakikisha malengo ya ndaki yanatekelezwa kwa ufanisi mkubwa

Akizungumza katika mkutano wa 18 wa Bodi hiyo, Dr Mbwile amesema wanatambua kazi kubwa inayofanywa na walimu na wafanyakazi wengine na kwamba licha ya wingi wa wanafunzi Ndaki ya Tiba ya Wanyama na Sayansi za Afya imeendelea kufanya vizuri na kukiletea chuo heshima kubwa

Aidha Dr Mbwile amewaasa wafanyakazi wa ndaki hiyo kuendelea kujitoa kwa nguvu kubwa kutimiza majukumu yao hasa katika kipindi hiki ambacho elimu ya afya ya binadamu na wanyama ni muhimu kwa ustawi wa jamii yetu. Mwenyekiti huyo amesema ili kutoa mchango mkubwa katika ujenzi wa taifa, ni lazima ndaki ijikite na kuweka nguvu katika kutatua changamoto za jamii hasa kwenye suala la magonjwa ya wanyama na afya ya jamii.

Bodi ya Ndaki (College Board) ndio chombo cha juu kabisa cha uawala katika katika ngazi ya ndaki kinachosimamia na kuhakikisha utendaji bora wa utekelezaji wa majukumu ya kila siku. Kikao cha 18 cha bodi hiyo kimefanyika tarehe 30/04/2021 katika ukumbi wa mkutano wa SACIDS uliopo kwenye moja ya majengo ya ndaki hiyo. Katika mkutano huo mambo mbalimbali yamejadiliwa yakilenga kuongeza ufanisi katika kutoa elimu na kufanya tafiti zinazolenga kutatua matatizo mbalimbali ya jamii.

Bodi 1

Washiriki wa mkutano wa 18 wa Bodi ya Ndaki ya Tiba ya wanyama na Sayansi za Afya wakiwa katika picha ya pamoja

 

Related Posts