Je, umewahi kuona mbwa au paka akifanyiwa upasuaji wa kufunga ama kutoa kizazi ili wasizaliane badala yake waendelee kufanya shughuli zao kwa ufanisi?

Basi hilo lipo nawe kama una paka wako jike, kwa mfano na hutaki azae inawezekana. Hayo, pamoja na mengine yamedhihirika kwenye maonesho ya maadhimisho ya Siku ya Madaktari wa Wanyama Duniani yaliyofanyika kitaifa katika Viwanja vya Mwembetogwa mjini Iringa.

Dkt. Aloyce Bunyage, Mtaalamu wa wanyama kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo amesema kuwa upasuaji wa wanyama hao ni ombi la wafugaji kutaka mbwa na paka watolewe vizazi ili wasizae tena.

Related Posts