Rais Samia Suluhu amteua Prof Erick Komba TALIRI

Eric Komba

Eric Komba

Prof Erick Vitus Komba

 

HONGERA

Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan amemteua Profesa Erick Vitus Komba kuwa Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI). Taafrifa iliyotolewa hivi karibuni na ikulu Dodoma imesema kuwa Prof Komba anachukua nafasi ya Dr Eligy Shirima ambaye amestaafu. Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa uteuzi wa Prof Komba umeanza tarehe 20 April 2021

Kabla ya uteuzi huo Prof Erick Komba alikuwa Profesa na Mhadhiri mwandamizi wa epidemiolojia ya magonjwa ya wanyama katika Idara ya Tiba ya Mifugo na Afya ya Umma katika Ndaki (College) ya Tiba ya Mifugo na Sayansi za Afya ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo.

Ndaki ya Tiba ya Mifugo na Sayansi za Afya inamtakia Prof Komba mafanikio katika utendaji wa kazi yake mpya.

Related Posts